OFISI YA AFISA MDHAMINI - ORTMSMIM (OFISI KUU PEMBA)
Ofisi ya Afisa Mdhamini ni kiungo kati ya Taasisi za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ zilizopo Pemba ikiwa na jukumu kuu la kuratibu na kusimamia kazi zote za Ofisi kwa upande wa Pemba.
UONGOZI
Kiongozi mkuu (Afisa Mdhamini) wa shughuli za ORTMSMIM kwa upande wa Pemba niNd. THABIT OTHMAN ABDALLA
MAJUKUMU YA OFISI YA AFISA MDHAMINI (KWA UPANDE WA PEMBA)
- Kuratibu shughuli zote zinazofanywa na ORTMSMIM.
- Kuratibu na kuwasilisha ripoti au taarifa za utekelezaji za kila robo, nusu na mwaka kwa Katibu Mkuu wa ORTMSMIM.
- Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
- Kuratibu taarifa za bajeti na hotuba ya makadario ya mapato na matumizi.
- Kuratibu,kushauri,kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Serikali za mitaa na Mamlaka zake.
- Kufuatilia na kukagua utendaji wa Serikali za Mitaa katika kutoa huduma.
- Kuimarisha utawala bora na kuimarisha uwezo wa Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma.