IDARA YA URATIBU IDARA MAALUM

Ofisi ya Uratibu Idara Maalum za SMZ inajukumu la kuratibu na kusimamia kazi za Idara Maalum za SMZ zikiwemo za utekelezaji wa sera mipango mikakati ya maendeleo, tafiti pamoja na kutoa miongozo kwa Idara Maalum na usimamizi wa Mahakama ya Rufaa za Idara Maalum za SMZ.

Aidha Idara inajukumu la kisera kwa kushirikiana na Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ juu ya masuala ya kiutumishi maslahi kuwajengea uwezo maafisa na wapiganaji kiutendaji na kuratibu masuala ya mashirikiano ya kiulinzi, kimichezo, operation maalum na mafunzo ya pamoja na utekelezaji wa maelekezo yote yatakayotolewa na Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za SMZ.

HISTORIA FUPI YA OFISI YA URATIBU

Ofisi ya Uratibu Idara Maalum za SMZ ilianzishwa mnamo miaka ya 1980 ambayo shughuli zake zikisimamiwa na mratibu Idara Maalum tokea kuanzishwa kwake hadi mwaka 2017, Ofisi hii imekuwa ikiongozwa na mratibu ambae huteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Idara Maalum za SMZ kwa mujibu wa sheria.

Kuanzia tarehe 2/10/2017 kwa mara ya kwanza uteuzi wa kiongozi wa Ofisi hii ulifanywa kwa mamlaka ya Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi chini ya kifungu cha 53 (a) cha katiba ya Zanzibar na kifungu cha 12 (2) cha sheria ya Utumishi wa Umma.

UONGOZI

Mratibu wa Idara ya Uratibu wa Idara Maalum ni: ...................

MAJUKUMU YA IDARA YA URATIBU

Mabadiliko haya ya mamlaka ya uteuzi wa kiongozi wa ofisi hii yanalazimisha kutathiminiwa upya kwa kazi za ofisi zinazofanywa hivi sasa ili ziendane na hali ya ofisi kulingana na taasisi sahihi ya majukumu ya Idara Maalum za SMZ.

Ofisi ya Uratibu ya Idara Maalum za SMZ kwa sasa inamajukumu yafuatayo:

  1. Kuratibu mafunzo ya kiulinzi na kiusalama ndani na nje ya nchi.
  2. Kuratibu mahusiano na mashirikiano kwa vyombo vya kiulinzi na kiusala baina ya SMT na SMZ.
  3. Kufanya uperesheni maalum kwa kazi za ulinzi na ujenzi wa taifa.
  4. kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo mikakati,sera,miongozo ya bajeti na tafiti za Idara Maalum pamoja na kutoa miongozo ya Serikali kwa Idara Maalum kwa idhini ya Wizara.
  5. Kuratibu uandaaji na ushiriki wa michezo kwa upande wa kanda ya Zanzibar BAMATA.
  6. Kuratibu program za mafunzo ya muda na mrefu kwa viongozi maafisa na maaskari kwa kushirikiana na Idara husika.
  7. Kupokea na kusimamia maelekezo na maagizo yeyote yanayohusu Idara Maalum kutoka kwa Kamanda Mkuu wa Idara Maalum.

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

3769455
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
121
366
2063
4655
3769455