IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI:
MUUNDO
1. MKURUGENZI
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi ni Ndugu JUMA NYASA JUMA.
MAJUKUMU
- Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali Watu na Utawala kwa wizara husika.
- Kusimamia makujumu ya vitengo vilivyo chini ya Idara.
- Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Wizara.
- Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji.
- Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa matakwa ya sheria au maagizo maalum.
- Kuratibu masuala mtambuka yakiwemo (Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya hali ya nchi, mambo ya idadi ya watu).
- Kutoa huduma za kitaalamu na huduma za manunuzi na uhifadhi wa vifaa kwa ajili ya Idara nyengine.
- Kutoa huduma za uhasibu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, mapato na matumizi, ulipaji wa mishahara na matayarisho ya mafao ya uzeeni.
- Kuandaa na kusimamia mpango kazi wa Idara.
- Kuandaa na kusimamia bajeti ya Idara.
- Kufanya kazi nyenginezo kama zitakavyoelekezwa na Uongozi wa Wizara kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za kazi.
2. KITENGO CHA UENDESHAJI
Kinaongozwa na Ofisa Utawala Mkuu.
MAJUKUMU
- Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi.
- Kusaidia kusimamia nidhamu ya wafanyakazi.
- Kuainisha matatizo ya wafanyakazi.
- Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya wizara ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano.
- Kusimamia majengo na mali nyengine zisizohamishika.
- Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Wizara.
- Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
3. KITENGO CHA UTUMISHI
Kinaongozwa na Ofisa Mkuu Utumishi.
MAJUKUMU
- Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote kulingana na mahali alipo.
- Kukusanya takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
- Kusaidia kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
- Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
4. KITENGO CHA UTUNZAJI KUMBUKUMBU
Kinaongozwa na Ofisa Kumbukumbu Mkuu.
MAJUKUMU
- Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
- Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
- Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
- Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
- Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
- Kufanya kazi nyengine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.