Kikosi cha Valantia

 

Kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ) ni miongoni mwa Idara tano Maalum za Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilicho chini ya Afisi ya Rais Tawala za mikoa na Idara Maalum za (SMZ)

Kikosi cha Valantia Kimeanzishwa Kwa Sheria Namba 5 ya Mwaka 2004 na kwa mujibu wa Sheria hiyo kikosi kina majukumu ya kueka amani na utulivu katika nchi, kupambana na janga lolote litakalo ikumba jamii kulinda Viongozi na mali za serekali na kufanya kazi za kijeshi kwa madhumuni ya kuzuia hali inayohatarisha ulinzi na usalama.

HISTORIA YA KIKOSI CHA VALANTIA

Katika mwaka 1957 jitihada za kupigania Uhuru zilipoibuka vyama siasa viliundwa ambapo chama cha Afro Shirazi Party (ASP) kiliundwa kutokana na muungano wa chama cha Afro Association na Shirazi Association, Afro Shirazi Party kilikua ni chama kilichodai uhuru kutoka kwa wakoloni wa kisultan.  Vijana nao walijitolea katika shughuli mbali mbali za Afro Shirazi Party.

Kwa wakati huo wito kwa vijana ulitolewa kwa ajili ya chama hasa kupitia katika mikutano ya hadhara kwa ajili ya ulinzi wa chama, majengo na mikutano ya chama. Afro Shirazi Party ikaamua kuhamasisha vijana wake wakaunda umoja wa vijana wa ASP na ndani yake wakaunda vijana wa Valantia.

Vijana wa Valantia walikua Imara kisiasa na pia kua waaminifu kiasi cha kupewa kazi za kukusanya michango ya fedha kwenye mikutano ya hadhara ya chama bila ya kutoa stakabadhi na kuziwakilisha kamili kwa mkusanyaji mkuu wa fedha hizo. Vijana hao walifanya Shughuli hizo kwa uaminifu mkubwa usiokua na dosari na pia walijitolea katika shughuli za kudai uhuru wakiungana na viongozi wao

Mara baada ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 chama cha ASP kiliendeleza Valantia kama chombo chake cha Ulinzi ingawa baadhi yao walipelekwa jeshini na kwenye vikosi vyengine vya Ulinzi kwa kupata ajira, na baadhi yao kuingizwa kwenye Utumishi wa Serekali, katika mpango huu vijana wengi walishawishika kujiunga na Valantia.

Hali hii ilizi kushamiri zaidi na zaidi kwenye mwaka 1966 ambapo kambi za vijana zilianzishwa(Youth Camps) kwenye mikoa mbali mbali Unguja na Pemba lengo kuu ilikua nikuwataarisha vijana kuja kushika nafasi mbali mbali za uongozi katika jamii ya Serekali

Ukweli ulio dhahiri ni kwamba  vikosi ikiwemo vile vya SMT na SMZ  kama vile JWTZ,JKU,KMKM vilipoanzishwa vilipoanzishwa wapiganaji wengi waliojiunga walichukuliwa kutoka vijana hawa wa Valantia.

Mnamo mwaka 1971 serikali ilipitisha Decree iliyoitwa Youth Camp Decree 1971 ambayo iliweka kikosi maalum cha kujitolea kua ni sehemu ya vikosi vingine vya Serikali ambacho kwa wakati huo kiliitwa Peoples Voluntary Brigade na kuekwa kwenye sheria Nam 8 ya mwaka 1982. ambayo ilisomeka kama ifuatavyo:-

 An organized group of selected people in Zanzibar other than the police, the defense force, the JKU and Chuo cha mafunzo operating with the authority of the government of Zanzibar specifically charged with the task of participating and aiding in any law enforcement exercise aimed at the protection of the country, the people of their property in relation to any contravetion of offences provided for under this act. ( Voluntary special brigade act of 1982, section 2)         

Na kwenye Ibara ya 3 (3) (a-c) ya sheria hiyo itatoa majukumu yafuatayo:-       

To assist and aid the party and the government in the fight against commodity racketeers and loiterers and corruption in general and in public instruction. Any activity which is incompatible with the political, economic or social goal and aspiration on the nation.

To undertake such training in the use of arms and weapons as may necessary forth the successful achievement of the objectives.

In the couse of discharging their functions, every member of the special voluntary brigade shall have the same power of arrest and search for breach of any provision of laws of the country(section 4 (1)).

kwa wakati ule kikosi hicho cha kujitolea kilitakiwa kusaidia serikali na chama tawala cha mapinduzi (CCM) ambacho kulikua ndicho chama pekee cha siasa.

Hatimae mnamo mwaka 2004 serikali iliifuta sheria ya zamani yaani ile ya Nam 8 ya mwaka 1982 na kueka sheria ya Nam 5 ya mwaka 2004 ya kikosi maalum cha kujitolea ikabadilika jina kuitwa kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ). Ndani ya Sheria hii mpya kikosi hiki kilijumuisha watumishi wa ajira na wa kujitilea wakawa ni Valantia wale waliostaafu katika utumishi wa Valantia ambao kwa sasa wameandikishwa kwa masharti ya kujitolea.

Katika hali hii majukumu ya Valantia yakatofautiana na yale ya kikosi maalum cha kujitolea ambapo kazi za kikosi cha Valantia zilipanuliwa na kuimarishwa kama ifuatavyo:-

a) Kushirikiana na vikosi vya Ulinzi na Usalama au taasisi nyenginezo katika katika Ulinzi wa Jamuhuri ya Muungano.

b) Kukabiliana na maafa yoyote yatajitokeza na kuathiri jamii.

c) Kulinda Mali za Serekali.

d) Kudhibibiti hali ya usalama na amani ndani ya nchi.                                                        

e) kufanya kazi za kiaskari kwa lengo la kudhibiti hali zisizo za kawaida kiulinzi na kiusalama.

f) kufanya kazi nyengine yoyote kama itakavyo tolewa au kuagizwa na Raisi au Waziri au Mamlaka yoyote iliyoteuliwa.

g) Katika kufanya kazi zake kila mtumishi wa Valantia atakua na nguvu na uwezo wa kukamata na kupekua kwa sababu ya tuhuma na uvunjaji wa sheria.

DIRA

Kikosi cha Valantia kuwa ni chombo muhimu na chenye ufanisi katika kutoa huduma ya Ulinzi wa Nchi, Raia na mali zao pamoja na kuhamasisha ushiriki wa kiulinzi katika Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

DHAMIRA

Ni kutoa Huduma ya Ulinzi kwa kushirikiana na taasisi nyengine za ulinzi na usalama  za  Serekali ya Zanzibar na serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kudumisha Amani na mshikamano wa Taifa. KVZ itajitahidi kutekeleza sera ya Taifa hususa sera ya kupunguza umaskini kupitia sera, mipango na majukumu yake ya kila siku ili kuchangia katika kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa jumla.

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

3769441
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
107
366
2049
4641
3769441