KATIBU MKUU AKIKATA UTEPE KUZINDUA MAGARI MANNE YA KVZ
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Nd. Issa Mahfoudh Haji amewataka wakufunzi wa Idara maalum za SMZ kuendeleza Mafunzo kwa Vikosi hivyo ili kuwaweka utayari kwa kulinda nchi yao. Ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Uongozi Mdogo mwaka 2026 katika chuo cha kufundishia Maaskari Pangatupu Wilaya kaskazini B.