• MAONESHO YA NANE NANENibu Waziri Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar MHE Hasaan Khamis Hafidh akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea bandani hapo.
  • MAONESHO YA NANE NANEMaafisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa Serikali Za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakitoa Elimu kwa Wanafunzi mbali mbali waliotembelea banda hilo.
  • UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA JKUKatibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Issa Mahfoudh Haji, amesema Serikali imejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika shughuli za uzalishaji za Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa lengo la kuongeza mapato.
  • MH WAZIRI ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE KIZIMBANI DOLEWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ameridhishwa na mafanikio ya Maonesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea Dole Kizimbani..
  • WAFANYAKAZI WA OR-TMISEMIMWafanyakazi wa Ofisi Y Rais Tawla Za MIkoa Serikali Za Mitaa Na Idara Maalum Za SMZ Wakiwaaga Watumishi waliomaliza muda wao katika Wizara hiyo.
OR-TAMISEMIM-HABARI

Angali Habari Zote

KATIBU MKUU AKIKATA UTEPE KUZINDUA MAGARI MANNE YA KVZ

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Nd. Issa Mahfoudh Haji amewataka wakufunzi wa Idara maalum za SMZ kuendeleza Mafunzo kwa Vikosi hivyo ili kuwaweka utayari kwa kulinda nchi yao. Ameyasema hayo kwa niab


Read More

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

MHE IDRISSA KITWANA MUSTAFA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Mh, Idrissa kitwana Mustafa, amesema ujenzi wa ofisi za masheha katika shehia itawawezesha kuongezeka uwajibikaji na wananchi kuwa huru pindi wanapofata huduma. Akitembelea ujenzi wa Ofisi ya Sheha shehia ya Ijitimai Mwanakwerekwe, amemtaka mkandarasi wa ujenzi huo Kikosi cha KVZ Kuharakisha ujenzi huo ili kuwawezesha masheha kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa wakaazi wao. Mkuu wa Wilaya ya Magharib 'B', Hamida Mussa Khamis, amesema anamatarajio kwa Masheha kuleta mabadiliko na kuwaondoshea mazingira magumu ya kazi waliyokumbana nayo hapo kabla. Mkandarasi wa ujenzi huo Mkuu wa Kikosi cha Valantia KVZ, Luten kanal Said Ali Shamhuna, amesema ujenzi huo umezingatia kiwango cha ubora kinachosimamiwa na Wakala wa Majengo ZBA na kuahidi kukamilika kwa wakati uliopangwa. Nae Sheha wa shehia ya Ijitimai Rashid Mwadini Omar, pamoja na mwananchi wa shehia hiyo wamepongeza hatua ya Serikali kuwajengea Ofisi ambazo zitaleta ufanisi na usiri wa kazi, tofauti na hapo awali. Jumla ya Ofisi 388 zinatarajiwa kujengwa kwa kila wilaya za Unguja na Pemba . Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano Or-tamisemim Zanzibar