Kikosi cha Zimamoto na Uokozi
Kikosi cha Zimamoto na Uokozi kimeanzishwa chini ya Sheria namba 7 ya mwaka 1999 iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Kikosi kina majukumu makuu yafuatayo hapa chini:-
- Kusimamia shughuli zote za uzimaji moto na Uokozi wa maisha na mali za watu pamoja na viumbe vyengine zinazosababishwa na majanga ya kimaumbile na yale yanayosababishwa na wanaadamu wenyewe.
- Kusimamia na kuhakikisha kuwa huduma za Zimamoto na Uokozi kwenye Viwanja vya Ndege Unguja na Pemba zinaenda sambamba na matakwa kulingana na sheria za kitaifa na kimataifa.
- Kusimamia na kutoa ushauri wa mafunzo mbali mbali ya kujikinga na majanga kwa wananchi na Taasisi mbali mbali za Serikali na za watu binafsi zilizopo nchini.
- Kusimamia na kutoa huduma mbali mbali kwa jamii kulingana na zana zilizopo Kikosini.
DIRA
Kutoa huduma za Uokozi na Uzimajimoto kwa haraka na Ufanisi.
DHAMIRA
Kuimarisha kwa huduma za Uokozi na Uzimajimoto kwa kulingana na matakwa ya Kitaifa na Kimataifa.